HabariMichezo

Ronaldo akiri Man United kumemkomaza kiakili

Cristiano Ronaldo amesema changamoto alizopitia Manchester United zimekuwa sehemu ya ukuaji wake na kwa sasa amekuwa bora zaidi kwa sababu yao, nyota huyo amezungumza hayo kwa mara ya kwanza tangu kuondoka kwake.

Mreno huyo mkataba wake na United ulivunjwa kufuatia mahojiano yake na mtangazaji, Piers Morgan yaliyo jaa shutuma kwa Kocha, Erik ten Hag na wamiliki wa Klabu hiyo.

Akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Ureno, Ronaldo amesema ”Wakati mwingine, unapaswa kupitia baadhi ya mambo ili kuona nani yuko upande wangu. Hakuna shaka kama nitasema nilikuwa katika hali mbaya, lakini hakuna muda wa kujutia, maisha yanaendelea, kufanya vizuri ama laa ni sehemu ya ukuaji wangu.”

“Tunapokuwa kileleni mara nyingi hatuwezi kuona kilicho chini. Sasa, nimejitayarisha zaidi na nimejifunza jambo ambalo lilikuwa muhimu, kwa sababu sikuwahi kupitia haya yaliyo nikuta miezi michache iliyopita. Kwa sasa nimekuwa bora.”

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents