Bongo5 ExclusivesHabariLifestyleMichezo

Ronaldo anaiuza Ndege yake, imekuwa ndogo kwa matumizi

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ambaye ametangaza kuondoka katika klabu hiyo Mreno Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka (37) ameiweka ndege yake sokoni kwa kuwa imekuwa ndogo mno kwake.

Ndege hiyo aliyoinunua mwaka 2015 na ilimgharimu mchezaji huyo wa Ureno euro milioni 20 ambayo ni zaidi ya Tsh 48,015,144,140/= alipokuwa akiichezea Real Madrid, sasa ni ndogo mno kwake kutokana na ongezeko la familia yake na watu wake wa karibu ambao hupendi kutembea nao.

Hayo ni kwa mujibu wa ESdiario, ambaye anadai kuwa nia yake sasa ni kupata ndege kubwa zaidi. Kulingana na habari hii, Cristiano hukodisha ndege yake ya kibinafsi wakati haitumii, kwa kiwango cha kati ya euro 6,000 na 10,000 ambazo ni sawa na Tsh 24,007,572/= kwa kila saa ya safari.

Kwa pesa atakazopata kutokana na mauzo hayo, nyota huyo wa Ureno anapanga kuongeza kama sehemu ya ununuzi wa ndege mpya, ingawa bado hajaamua ni ipi anaitaka.

Ndege yake ya sasa inaweza kubeba abiria kumi pekee, uwezo mdogo kwa familia yake, inaelezwa kuwa Inasafiri 900km kwa saa .Ndege hiyo inaelezwa kuwa ya kifahari zaidi hadi baadhi ya vitu ambavyo vilikuwepo kwenye Ndege hiyo havikutosha kwa matumizi ya Ronaldo na familia yake vitu vingine ilibidi viongezwe kukidhi mahitaji yake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents