Ronaldo atarudi Sporting – Mama

Kuna watu wachache tu ammbao wanaweza kumwambia nini cha kufanya Cristiano Ronaldo,lakini mama yake na mchezaji huyo , Dolores Aveiro amesema kuwa atamshauri mtoto wake kurejea Sporting msimu huu wa majira ya joto.

Ingawaje Ronaldo anaongoza kwa kufunga magoli Serie A msimu huu huku akifikisha jumka ya mabao 100 ndani ya Juventus baada ya ushindi wa 3-1  siku ya Jumatano dhidi ya Sassuolo lakini bado anapitia wakati mgumu msimu huu kutomalizandani ya nafasi nne za juu kwenye msimamo ikiwa moja ya changamoto zinazomkabili.

“Nitazungumza naye Cristiano kumrudisha, msimu ujao atakuja kucheza Sporting,”- amesema mama huyo.

Ronaldo, 36, amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake na Juventus, lakini amehusishwa na kujiunga na Sporting na Manchester United.

Related Articles

Back to top button