Ronaldo avunja masharti Italia, Rais Juve awataka Mawaziri hawa kujibu

Waziri wa michezo nchini Itali amesema kuwa, Cristiano Ronaldo huwenda akawa amevunja sheria za afya wakati aliporejea Italia mara baada ya kupimwa na kukutwa na virusi vya Corona alipokuwa Ureno.

Mshambuliaji huyo wa Juventus alirejea Itali na ndege binafsi siku ya Jumatano na kujiweka karantini nyumbani kwake.

Vincenzo Spadafora aliulizwa katika mahojiano yake na kipindi cha radio ikiwa Ronaldo amevunja sheria za afya kwa kufanya hivyo na ndipo Waziri huyo wa michezo akajibu ”Ndiyo nadhani hivyo kama hakukuwa na idhini maalum kutoka katika mamlaka ya afya”

Hata hivyo rais wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli amemkingia kifua mchezaji wake kwa kusema hakuna sheria iliyovunjwa.

“Lazima upige simu kwa Waziri wa Afya na Waziri wa Mambo ya Ndani uwaambie waeleze kitu gani kimekiukwa,” amesema Agnelli.

Siku ya Jumatano klabu ya Juventus ilisema Ronaldo amerejea kwa ndege ya matibabu iliyoidhinishwa na maafisa wa afya.

Ronaldo alicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Hispania na wa UEFA Nations League akiwakabili Ufaransa na kushindwa kucheza dhidi ya Sweden kutokana na kukutwa na virusi vya Corona wakati Ureno ikichomoka na ushindi wa magoli 3 – 0 katika mechi hiyo ya siku ya Jumatano.

Imeandikwa na Hamza Fumo, Instagram @fumo255

Related Articles

Back to top button