HabariMichezo

Ronaldo goli amepewa kama zawadi- Kocha wa Ghana

Kocha wa Ghana Atto Oddo amemkosa mwamuzi kwa kutoa adhabu ya mkwaju wa penati ambayo imempa nafasi Cristiano Ronaldo kuweka rekodi ya magoli katika mchuano wa Kombe la Dunia kwa kuiita hatua hiyo kama zawadi maalumu.

Ushindi wa jana kwa Ronaldo unamfanya awe mchezaji pekee wa kwanza wa kiume kuibuka na ushindi katika michuano mitano tofauti ya Kombe la Dunia.

Katika mechi hiyo Ureno Ureno iliibuka na ushindi wa magoli 3-2 mbele ya Ghana.

Kocha Addo amesikika akisema ” kama mtu amefunga goli anastahili pongezi. Lakini goli hili kwa kweli ilikuwa zawadi maalum. Sina zaidi la kusema, ilikuwa ni zawadi maalum kutoka kwa kocha.”

Ukosoaji huo wa moja kwa moja wa Addo kwa mwamuzi Ismail Elfath unaweza kumwingiza matatizoni na Shirikisho la Kandanda ulimwenguni FIFA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents