Ronaldo mbadala wa Mbappe PSG

Matajiri wa Ufaransa klabu ya Paris Saint-Germain wamewasiliana na mchezaji Cristiano Ronaldo kuangalia uwezekano wa kumng’oa ndani ya Juventus, hii ni kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania.

Thomas Tuchel admits 'maybe I have a new contract now' after Chelsea won the Champions League | Daily Mail Online

Inaaminika kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 36, yupo huru kama ataamua kundoka kwa wa babe hao wa Serie A msimu huu kutokana na ukosoaji mkubwa dhidi yake juu ya kushindwa kuibeba timu hiyo pale ilipokuwa ikiwania ubingwa wa Coppa Italia na Italian Super Cup.

Mreno huyo ambaye amefunga jumla ya magoli 36 kwenye mashindano yote ameshuhudia ubingwa ligi kuu ukienda kwa Inter Millan huku wakishindwa kufanya maajabu kwenye michuano ya UEFA Champions League kwa kutolewa mapema tofauti na matarajio ya waliowengi.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Hispania zinadai kuwa PSG imewasiliana na mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Real Madrid kuangalia uwezekano wa kumsajili.

Hata hivyo inadaiwa kuwa kutaka kusajiliwa kwa Ronaldo na kama mbadala wa kuondoka kwa nyota Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 22.

Related Articles

Back to top button