Habari

Rose na James Chuchu wana tuhuma, wasimamishwa kazi

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Uyui mkoani Tabora amewasimamisha kazi Rose Shirima, aliyekutwa na tuhuma ya matumizi ya lugha isiyo na staha mahali pa kazi na James Chuchu aliyekutwa na tuhuma ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kuleta taharuki katika jamii.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Januari 25, 2023, kufuatia uchunguzi uliofanywa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Halmshauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora, baada ya video kusambaa mitandaoni ikiwaonesha Rose Shirima ambaye ni Muuguzi Mkunga na Getogo James Chuchu ambaye ni Mteknolojia wa Maabara, wakibishana kuhusu vipimo vya malaria vilivyoisha muda wake

Aidha uchunguzi huo pia umebaini kuwa hakuna mgonjwa aliyepimwa malaria kwa kutumia vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi licha ya uwepo wa vitendanishi vilivyoisha muda wake wa matumizi tangu mwezi Agosti 2022 na kwamba zahanati hiyo ina vitendanishi ambavyo vitaisha muda wake Aprili na Desemba 2023.

Mbali na hayo uchunguzi pia umebaini kuwa kuna mahusiano yasiyoridhisha kwa baadhi ya wafanyakazi katika zahanati hiyo, usimamizi wa kituo usioridhisha na kwamba watumishi wanne wa zahanati hiyo wamekutwa na tuhuma za kujibu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents