RRECAP: Rayvanny akili kubwa kutumbuiza michuano ya CHAN, Ganda amefunika – El Mando

Kupitia kwenye kipindi chake cha @recap_mando @el_mando_tz amemzungumzia mkali Rayvanny ambaye amefanya vizuri kwenye Remix ya Ganda ya Mzee wa Bwax & D Voice.
Anasema kuwa Rayvanny amefanya vizuri sana kwenye ile Remix lakini ameshangaa kutokuwepo kwenye ngoma na pia yeye kupost kwenye akaunti yake ya Youtube licha ya kuwa D Voice kapost kwake.
Pia @el_mando_tz ametusanua kuwa Rayvanny atakuwa miongoni mwa Wasanii watakaotumbuiza Jumamosi Tarehe 2 kwenye uzinduzi wa michuano ya CHAN katika Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar Es Salaam.
Rayvanny amepata nafasi hiyo adhimu kabisa ambayo itaendelea kumtangaza Kwa Ukubwa nje ya mipaka ya Tanzania.
Michuano hiyo Itaonekana duania nzima hivyo ni nafasi kwake aendelee kuutangaza muziki wake na muziki wa Tanzania, Rayvanny ana akili maana sehemu nyingi nyetu yeye huwa wa kwanza.
Uchambuzi mzima upo katika akaunti yetu ya YouTube ya Bongofive.
Cameraman & Editor @johnbosco_mbanga






