Habari

Ruto awatoa hofu wa Kongo, awaahidi amani

Rais wa Kenya William Ruto amesema leo kuwa wanajeshi wa jumuiya ya Afrika Mashariki “watahakikisha uwepo wa amani” mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo inakabiliwa na mashambulizi kutoka kundi la waasi wa M23.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Kinshasa, Ruto amesema wanajeshi hao wa kikanda “watatekeleza amani kwa wale wenye nia ya kuleta ukosefu wa utulivu.”

Rais huyo wa Kenya ameeleza kuwa, anafahamu juu ya uwepo wa vikosi vyengine vya kulinda amani mashariki mwa DRC, japo amesema wanajeshi hao wa jumuiya ya Afrika Mashariki watapiga jeki juhudi za kulinda amani. Wanajeshi wa Kenya, waliotumwa kama sehemu ya kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki, waliwasili hivi karibuni katika eneo hilo lenye machafuko.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents