Saa ya Hitler iliyouzwa dola milioni 1.1 mnadani, yauzwa tena


Saa ya mkononi iliyosemekana kuwa ni ya aliyekuwa kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler imeuzwa kwa dola milioni 1.1 katika mnada nchini Marekani.
Saa hiyo, inayoitwa Huber Timepiece, iliuzwa kwa mnunuzi ambaye hajuliikani. saa hiyo imeandikwa Herufi -AH ( kwa kirefu-Adolf Hitler).
Mauzo ya saa hiyo yalipingwa na viongozi wa Kiyahudi kabla ya Mnada huo wa Kihistoria kufanyika -Alexander Historical Auction huko Maryland.
Hatahivyo, kampuni iliyonunua iliviambia vyombo vya habari vya Ujerumani kwamba walikuwa wanajaribu kutunza historia.
Adolf Hitler aliiongoza Ujerumani chini ya utawala wa Nazi kuanzia mwaka 1933 hadi 1945.Watu zaidi ya milioni waliuawa kikatili wakati wa utawala wake. huku ikielewa kuwa zaidi ya Watu laki sita kati yao waliuawa tu kwasababu walikuwa ni Wayahudi.
