Fahamu

Sababu ya China kuongeza idadi ya watoto kuzaliwa kutoka mtoto mmoja hadi watatu

China sasa imewaruhusu watu kuwa na hadi watoto watatu baada ya kupungua kwa kiwango cha watoto wanaozaliwa nchini humo.Hatua hiyo ni mabadiliko makubwa ya kisera kwa serikali ya nchi hiyo.

Shirika la habari linalomilikiwa na serikali Xinhua, limesema uamuzi huo ulitangazwa siku ya Jumatatu katika mkutano wa viongozi wakuu wa chama cha kikomunisti .

Tangazo hilo linajiri baada ya matokeo ya hesabu ya watu inayofanyika kila baada ya miaka kumi kuonesha kwamba idadi ya Wachina ilisajili ukuaji mdogo sana katika miongo iliyopita.

Hatua hiyo imeishinikiza Beijing kubadilisha sera ili kuwauhusu watu kuwa na watoto watatu.

China ilifutilia mbali sera yake ya mtoto mmoja mnamo 2016, na kuibadilisha na kikomo cha watoto wawili ambacho kimeshindwa kusababisha kuongezeka kwa idadi ya watu .

Gharama ya kulea watoto katika miji imezuia wanandoa wengi wa China kuza watoto zaidi.Hatua hiyo ya hivi karibuni iliidhinishwa na Rais Xi Jinping katika mkutano wa viongoziwakuu wa kisiasa shirika la habari la serikali limesema Kutakuwa na “hatua za kuunga mkono, ambazo zitasaidia kuboresha muundo wa idadi ya watu wa nchi yetu, kutimiza mkakati wa nchi kukabiliana kikamilifu na idadi ya watu waliozeeka na kudumisha faida na utoaji wa nguvu azi “, Xinhua ilisema.

Lakini wataalam wengine walikuwa na wasiwasi juu ya athari ya sera hiyo”Ikiwa kulegeza sera ya idadi ya watoto kungekuwa na ufanisi, sera ya sasa ya watoto wawili inapaswa kudhibitishwa kuwa na ufanisi pia,” Hao Zhou, mchumi mwandamizi huko Commerzbank, aliambia Reuters.”Lakini ni nani anataka kuwa na watoto watatu? Vijana wanaweza kuwa na watoto wawiliiwapo ni wengi. Suala la msingi ni gharama ya maisha ni kubwa sana na shinikizo za maisha ni kubwa sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents