Sababu ya Christina Shusho kutengana na Mumewe, Maisha yake halisi sasa

Mwimbaji tajika kutoka Tanzania Christina Shusho amefunguka kuhusu kutengana na mumewe ili aweze kuzingatia wito wake.
Nyota huyo aliyevuma na wimbo wa Shusha Nyavu alikuwa kwenye mahojiano na New Jerusalem Church TV, ambapo alisema alikuwa na ndoto ambayo alitarajia kuona ikiwa hai na kufichua kuwa walitengana kwa kuelewana. “Sijawahi kuwa fake, wala sidanganyi, ukweli ni kazi tu, hakuna tofauti zaidi ya hiyo, kazi aliyonipa Mungu msimu huu haiwezi kuniruhusu kubaki pale nilipokuwa. kuondoka kwenda kutekeleza jukumu hilo,” alisema. Pia alishikilia kuwa yeye sio mchungaji na alionyesha kutofurahishwa na kuitwa mhubiri.
Pia alifichua kwamba anataka kufikia kila kitu alichokusudia kufanya na akafichua kwamba anawakuza wachungaji katika maisha yake.
Mimi ni mtu mwenye ndoto. Kuna kitu lazima nione. Sipendi watu wakiniita mchungaji. Nafikiri nina zaidi ya lazima nifanye,” aliongeza. Shusho pia alisimulia kuwa alimwomba mume wake amwachie ili aende kutimiza wito wake, na alifichua kuwa bado walikuwa na maelewano mazuri. Pia alipinga kuwa Mungu anaweza kumpa mwanamume na mwanamke wito unaohusiana na akasema kila mtu ana njia zake za kufuata hata kama wanasaidiana.
Ufichuzi wake ulisababisha hisia tofauti mtandaoni. Wengine walihoji kwa nini hangeweza kutimiza wito wake pamoja na mume wake, huku wengine wakimtakia heri njema.
Imeandikwa na Mbanga B.