Burudani

Sababu ya Zuchu kurushiwa vitu jukwaani,Mbeya hii hapa,aombe radhi(Video)

Kupitia kwenye kipindi chake cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumzia tukio la Zuchu kurushiwa mawe na mashabiki show ya Wasafi Festival Mbeya.

Anasema kuwa anapinga na anakemea mashabiki kufanya vitendo kama vile kwa wasanii wao maana inaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo msanii kuumizwa.

Anaongeza kuwa tukio lililotokea haliwezi kutokea bila sababu na sababu ilianzia kwa Zuchu mwenyewe kwa kuonyesha kidole kwa mashabiki.

Kwa upande wa msanii pia ni jambo na kukemewa maana sio kitendo kizuri kuwafanyia mashabiki wako waliolipa pesa kuja kukutazama.

Msanii atapokuwa jukwaani maana pale ndio ofisini kwake anatakiwa awe na uwezo wa ku-control hasira na feeling zake na pia awe na uwezo wa ku-handle Audience yake.

Wasanii wote wakubwa hata akina Diamond, Alikiba washakutana na hayo mambo mengi sana na mara zote wamekuwa wakikabiliana nazo bila kutukanana na mashabiki wao na ndio maana wapo hapo walipo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents