Siasa

Sababu za Bobi Wine kuiondoa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Uganda mahakamani (+ Video)

Kiongozi wa chama cha upinzani cha National Unity Platform (NUP) Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine ameondoa mashitaka yake ya kupinga uchaguzi wa Urais wa Uganda aliyowasilisha dhidi ya Rais Museveni.

Alitaja hatua ya jaji kukataa kuongezea ushahidi zaidi uliyowasilishwa na timu yake kama sababu ya kuondoa kesi hiyo.

Pia ameongezea kuwa suala hilo litaamuliwa na wananchi lakini akatoa wito kwa wafuasi wake kutojihusisha na ghasia.

Hatua ya Bobi Wine inakuja siku moja baada ya Rais Museveni, Tume ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu kuwasilisha hati zao za kiapo 185 kujibu sababu 53 ambazo timu ya wanasheria ya NUP ilikuwa imeibua kuthibitisha kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa wizi, na haukuwa huru na wa haki.

Chama cha Rais Museveni pia kimetuma ujumbe wa Twitter kuwa Museveni amepata ushindi katika kesi hiyo.

Siku ya Jumapili , mawakili wa chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) walisema Bobi Wine atakabiliwa na athari kubwa za kifedha ikiwa atathubutu kuondoa ombi la kupinga ushindi wa Bw Museveni kwenye Mahakama Kuu.

Bofya hapa chini kumtazama.

https://www.instagram.com/tv/CLoLamzhSLl/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents