Sababu za ‘Fei Toto’ kubaki Yanga

Kiungo fundi wa mpira, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amewajulisha wana Yanga kwamba bado yupo sana ndani ya Klabu hiyo kwani anafuraha.

Kauli hiyo ya ‘Midfilder’ wa Jangwani imekuja wakati akibadilishana mawazo na mashabiki zake kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter.

Akijibu swali la Shabiki yake, ambaye alimuuliza kama anampango wa kuichezea Klabu nyingine tofauti na Young Africans, Fei Toto amesema, “Kwa sasa nipo Yanga na naipenda, nina furaha pia” .

Akizungumzia malengo yake, amesema kwa sasa anataka kuisaidia Klabu yake ifanye vizuri, ichukue makombe mengi, nifanikiwe na timu ya taifa pia, na kimataifa zaidi.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button