Sababu za FIFA kufungua ofisi ndogo Rwanda baada ya kuzihamisha Ethiopia (+ Video)

Raisi wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani, FIFA, Gianni Infantino amezindua rasmi tawi la sgirikisho hilo katika mji mkuu wa Rwanda Kigali, limesema Shirikisho la soka nchini Rwanda.

Makao makuu ya tawi hilo la FIFA la maendeleo ya mpira wa miguu katika eneo hili la Afrika yalikuwa nchini Ethiopia, lakini baadae FIFA ikaamua kuyahamishia mjini Kigali.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katikati mwa mji wa Kigali, Bw Gianni Infantino aliambatana na wenyeji wake, Waziri wa mambo ya nje Vincent Biruta pamoja na Waziri wa michezo Aurore Munyangaju.

Kulingana FIFA tawi hilo litakuwa na jukumu la kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu yanafikiwa katika maeneo ya Afrika Mashariki na kati.

Pia litakuwa na jukumu la kupokea mikutano ya wajumbe wa FIFA katika eneo hilo na kutoa ushauri na taarifa kuhusu soka ya eneo hilo kwenye makao makuu yaFIFA yaliyoko Zurich nchini Uswiss.

Bofya hapa chini kuitazama video nzima.

https://www.instagram.com/tv/CLgWTVvhPPV/

Related Articles

Back to top button
Close