Sababu za Marekani kushindwa kuingilia, kifo cha mwandishi Khashoggi kuuliwa na mtoto wa mfalme Saudia Arabia (+Video)

Utawala mpya wa Marekani unatarajiwa kuchukua hatua dhidi ya ufalme wa Saudia na mrithi Mohammed bin Salman, huku Joe Biden akisema mara kwa mara kuwa atawawajibisha wakiukaji wa haki za binadamu.

Idara ya ujasusi ya Marekani hivi karibuni ilitoa maelezo ya kina juu ya mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi, ambayo Mohammed bin Salman amekwua akilaumiwa – mtoto wa mfalme wa Saudia- baada ya hatua inayofuata ya serikali ya Biden.

Siku ya Ijumaa, Rais Biden alimpigia simu Mfalme Salman bin Abdulaziz na kutahadharisha juu ya matokeo ya ripoti kuhusu mauaji ya Khashoggi.

Lakini ni nini kinachozuia Marekani kumuadhibu Mohammed bin Salman au kuweka vikwazo?

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya Ijumaa alizungumza na Mfalme Salman wa Saudi Arabia

Tangu Biden aingie madarakani, magazeti makubwa ya kimataifa yamezingatia uhusiano unaowezekana kati ya Saudi Arabia na utawala mpya ambao umeichukua Ikulu ya White House.

Wachambuzi wanasema kwamba wakati wanadiplomasia wa Marekani wanapotahadharishwa na Saudi Arabia, wanakumbusha kila mtu kwamba Ufalme ni mshirika wa Marekani.

Lakini maafisa wa Saudia wanachukua mtazamo tofauti, wataalam wanasema. Wanaamini kuwa Marekani ina ahadi ya kuchimba mafuta kutoka kwao na badala yake kuwapa usalama, ambayo imekuwa hivyo tangu kampuni ya kwanza ya Marekani kuingia mkataba wa mafuta na Saudi Arabia miaka ya 1930.

“Ikulu ya White House inajitetea dhidi ya madai kwamba Washington haikuweka vikwazo kwa mrithi wa ufalme wa Saudia,” The Guardian iliripoti.

Mohamed Bin Salman alikuwa akiungwa mkono na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump

Utawala wa Biden umesema kuwa haukuwa na haraka ya kuweka vikwazo dhidi ya Bin Salman, wakieleza uwezekano wa mazungumzo.

Mwanahabari wa Guardian amesema katika mahojiano na msemaji wa Ikulu ya White House Jen Psaki kuwa anaunga mkono uamuzi wa Washington kumlenga moja kwa moja Mohammed Bin Salman.

”Kuna namna nyingi za kuhakikisha kuwa tukio la Jamal Khashoggi halitokei tena, na tunatoa nafasi ya Ufalma na sisi kumaliza mgogoro,” Jen Psaki alinukuliwa na mwanahabari huyo.

Ofisi ya Biden imepuuza kukosolewa na viongozi wa chama cha Democratic, wanaotaka hatua zichukuliwe haraka dhidi ya Saudi Arabia.

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/tv/CL6r_BaBluc/

Related Articles

Back to top button