Michezo

Sadio Mane kutimkia Bayern Munich

Bayern Munich imekusudia kumsajili nyota wa Liverpool, Sadio Mane ikiwa kama lengo lao kuu kwenye dirisha la  usajili ujao wa kipindi cha majira ya kiangazi.

Mane amehusishwa kutaka kutimkia Bundesliga, na kwa mujibu wa gazeti la Bild, kutoka Ujerumani inadaiwa kuwa wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 tayari ameshakutana na uongozi wa klabu ya Beyern huko Mallorca kujadili usajili huo.

Hata hivyo kwa upande wake Sadio Mane ambaye mkataba wake wa sasa utafikia mwisho mwaka 2023, amesema kuwa atazungumzia hatma yake ya baadaye mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya Champions League dhidi ya Real Madrid wikiend hii.

Mane anaingia mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake Anfield baada miaka sita ndani ya Merseyside club.

Bayern Munich inamuhitaji Mane ili kuziba nafasi ya Robert Lewandowski ambaye inaaminika huwenda akajiunga na Barcelona baada ya kukubaliana mambo binafsi na miamba hiyo ya soka kutoka Hispania.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents