Michezo

Sakata la Kagere kutua Hispania lafikia patamu, wakala wake afunguka ”Wanataka kumsajili kwa muda…”

Wakala wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba ameeleza kuhusu mazungumzo yake na klabu ya Levante mpaka sasa yalipofikia.

”Levante wameniambia Meddie Kagere, wamemfuatilia walimuona Sevilla, timu inayotoka nchini kwao Hispania ilipokuja Bongo kucheza na Simba.” – amesema Gakumba

Patrick Gakumba ameongeza kuwa ”Na wakamfuatilia rekodi zake, wakaona ni mchezaji ambaye anafanya vizuri kote alikopita, iwe Rwanda, Kenya mpaka kuwa mfungaji bora.”

”Tumeshindwana kidogo tu, wao wanachotaka aende pale acheze mechi za majaribio, lakini Meddie Kagere sio mtu wa kucheza mechi za majaribio nimewaambia. Pesa waliyoniambia, wameniambia wanataka kumsajili kwa muda wa miezi sita ili wamuangalie. Nishawaambia mimi, Meddie Kagere atacheza hadiĀ  hawa watoto wadogo wanaomuita mzee hadi wenyewe watatoka.”

”Meddie Kagere tangu wameanza kumsema amezeeka miaka mitano imepita nyuma, na kila wanavyomuambia anafunga, mimi ninachoangalia ni magoli siangalii umri, nilisema sihitaji kumleta mchezaji ambaye atakuja kuniabiasha na heshima yangu ikashuka kisa ana umri mdogo.”

”Hawa Levante, wakati mwingine unajua hawa wanaleta dharau kwa Waafrika, wanasema sijui acheze miezi sita, mimi nimewaambia hiyo haiwezekani, mchezaji kama ni kusaini miaka miwili nipate mkwanja wa kutosha laa si hivyo nina ‘Big Boss Mo’ ambaye atanipa fedha ambayo nahitaji.”

Siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi juu ya klabu hii ya Hispania, Levante UD kuhusishwa na kutaka kumsajili mshambuliaji wa Simba SC, Meddie Kagere.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents