Habari

Sakata la ringtone:JMakamba awataka wasanii wawe na msimamo mmoja


Naibu waziri wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia mheshimiwa January Makamba ameubariki uamuzi uliochukuwa jana na wasaniii wa Tanzania wa kuyaandikia makampuni ya simu na yale yanayouza miito ya simu kusitisha mara moja matumizi ya nyimbo zao ndani ya siku saba.
Akiongea na Clouds Fm jana, Mheshimiwa Makamba amesema kwanza amefurahi kuona wasanii hao wamechukua hatua hiyo kwakuwa ni haki yao kudai kile wanachostahili kupata kutokana na matumizi ya kazi zao.
Hata hivyo ameonesha wasiwasi wake kuwa kusije kukatokea wasanii wachache ambao watakuwa tofauti na wenzao kwa kukubali nyimbo zao ziendelee kutumika.
Amesema hasara ya kitu kama hicho ni kuwa wale waliogoma watajikuta wakiumia kwa kutopata chochote kabisa baada ya kuvunja mikataba yao na makampuni ya simu kuendelea kutumia nyimbo za wasanii wachache watakaowasaliti wenzao.
Kutokana na wasiwasi huo Mheshimiwa Makamba amesema wasanii wote wanatakiwa kuwa na msimamo mmoja.
Ameongeza kuwa ili kusaidia mchakato wa wasanii kuanza kupata haki yao, ameigiza kufanyika kwa mkutano wiki hii utakaowakutanisha wadau wa biashara hiyo ili kupata muafaka.
Hii ndio barua iliyoandikwa na mwanasheria wa umoja wa wasanii hao inayoyataka makampuni ya simu kusitisha matumizi ya nyimbo zao kama ringtone.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents