
Mtangazaji mkongwe nchini Salim Kikeke ametangazwa rasmi kuwa mwanafamilia mpya wa Crown FM.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Big Boss wa Crown Alikiba ameshare ujumbe wa kumkaribisha Kikeke.
My Brother Salim Kikeke hii ilikuwa ndoto na maono tuliyokuwa nayo muda mrefu. Wakati unafanya maamuzi ya kurudi Nyumbani Tanzania tulipata nafasi ya kuzungumza na nikakueleza Kiu yangu yakutaka kufanya kazi na wewe Gwiji na Mtaalam wa Tasnia hii ya Habari Afrika na Dunia nzima.
Najua Simu zilikuwa nyingi sana lakini uliona CROWN ni sehemu sahihi sana kwako. Karibu kuwa Sehemu ya Historia tunayoenda kuiandika pamoja.
Nimekuvisha Taji na CROWN Media tunaamini Hesabu zetu za Kimkakati zimekaa sawa. Karibu sana Nyumbani CROWN FM na CROWN TV.
Imeandikwa na Mbanga B.