Samia aonya Majaji kukimbia wananchi mahakamani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya Majaji kutumia milango iliyopo kwenye jengo jipya la vituo vya Utoaji Haki, kukimbia wananchi wanaotaka huduma.

Rais, Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ameitoa kauli hiyo leo Oktoba 6, katika sherehe ya Uzinduzi wa Vituo Jumuishi wa utoaji Haki zinazofanyika Jijini Dodoma.

Jengo lina mlango mitano, naomba ikatumike kwa nia na madhumuni iliyokusudi wa na siyo kutumika kama upenyo wa Majaji na Mahakimu kuwakimbia wananchi wanaowasubiri kupata huduma” Rais Samia.

Aidha Rais Samia amesema kwamba fedha zikizotumika kujenga jengo la vituo hivyo (Bilioni 9), zimeonekana kutumika vyema kwani thamani yake inaoneka ikiwepo kutenga vyumba mbalimbali ikiwa na sehemu ya wamama kunyoyeshea watoto wakati wa usikilizwaji wa kesi.

BY: Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button