Michezo
Sanchez hawezi kujiunga Manchester United – Mino Raiola

Hatima ya mcheziji wa klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez ipomikononi mwa kiungo wa Manchester United, Henrikh Mkhitaryan hii ni kwa mujibu wa wakala, Mino Raiola.
Arsenal haitoweza kukamilisha dili la paundi milioni 35 la Sanchez hadi timu hiyo itakapo mpata, Mkhitaryan jambo ambalo mpaka sasa kunasubiriwa busara za mchezaji huyo kuamua.
Raiola amekiambia chombo cha habari cha The Times “Manchester United haitoweza kumsajili Sanchez hadi pale Mkhi atakaporidhia kujiunga na Arsenal.”
“Mkhi mpaka sasa bado hajaamua chochote. Mkhi yeye ndiyepekee atakaeweza kuamua kilichobora kwa Sanchez.”Amesema Mino Raiola.