Habari

Sasa ni mwendo wa kidigitali, Mchongo Kiganjani

KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mfumo wa aina yake wa kufanya mauzo wenye lengo la kurahisisha na kuongeza ufanisi wa mauzo yake kwa kuwapa wasambazaji wao (Stockists, Wholesalers & Bars) taarifa za kisasa kwa kutumia simu. Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za SBL kukumbatia maendeleo katika uendeshaji wake na mtindo wa biashara.

 

Programu iliyopewa jina la DIAGEO ONE itakuwa suluhu moja kwa wateja wa SBL na kuwezesha mageuzi ya kiwango cha kimataifa jinsi SBL inavyofanya biashara na wateja wao. SBL ilizindua mfumo huo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kwa wateja wake muhimu baada ya awamu ya majaribio iliyoanza Februari mwaka huu kumalizika kwa ufanisi.

 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Meneja Mawasiliano na Uendelevu wa SBL, Rispa Hatibu alisema, “SBL tumedhamiria kufanya mageuzi katika shughuli zetu za biashara, hii ni pamoja na kutumia teknolojia na ubunifu ili kuhakikisha kuwa kuna ufanisi katika namna tunavyofanya biashara. SBL ina nafasi kubwa katika sekta hii, na ndio maana tunasimamia ubunifu wa programu kama hizi.”

Aliongeza, “kiwango cha kazi iliyohusika katika kufanikisha jambo hili imekuwa muhimu kwa timu mbali mbali za SBL, EABL, na usaidizi mpana wa kampuni mama ya SBL ili kuhakikisha tunatekeleza kwa ufanisi programu hii mpya ambayo itabadilisha njia za kufanya kazi kwa wateja wetu”

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko ya Kidijitali wa SBL Chelu Mapolu alisema uzinduzi wa DIAGEO ONE kwa mkoa wa Dar es Salaam unafuatia mafanikio ya awamu ya majaribio ya mfumo huo, ambapo SBL imepima utendaji kazi na ufanisi wa mfumo huo kwawasambazaji na wateja mbalimbali jijini Dar es Salaam,” tumeifanyia majaribio na tunafurahia kuwaambia wasambazaji na wateja wetu kwamba mfumo huu utaleta mapinduzi makubwa kwa namna SBL inavyofanya mauzo. Kwa mfumo huu wa mauzo, wateja wetu watakuwa na taarifa muhimu zote kiganjani. Mfumo wa Diageo One ni rafiki kwa watumiaji na unafanya mchakato wetu wa uuzaji kuwa rahisi, mzuri na wa kufurahisha zaidi.”

 

Alibainisha kuwa, baada ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, matumizi ya mfumo wa DIAGEO ONE mchongo kiganjani utaanza kutumika kwa awamu nchini kote kwa wasambazaji wote wa bidhaa za SBL kuanzia mwezi Juni ambapo wateja wetu wote watapatiwa mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumohuo na njia bora wanayoweza kuutumia ili kurahisisha mchakato wao wa kuagiza na kufanya manunuzi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents