HabariSiasa

Scotland yataka kujitenga na Uingereza, yaanza kudai uhuru

Serikali ya Scotland imetangaza mipango ya kuandaa kura ya pili ya maoni kuhusu uhuru wa Scotland Oktoba mwaka ujao.

Waziri kiongozi wa Scotland Nicola Sturgeon ameapa kuchukua hatua ya kisheria kuhakikisha kura hiyo inafanyika kama serikali ya Uingereza itajaribu kuizuia.

Sturgeon alizungumza wakati serikali ya Uingereza, inayoongozwa na chama chake kinachounga mkono uhuru cha Scotland National, kuchapisha muswaada wa kura ya maoni unaoweka wazi mipango ya kufanyika kura hiyo ya kujitenga na Uingereza mnamo Oktoba 19, 2023.

Lakini pia alisema atamwandikia barua Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kupata idhini ya kuandaliwa kura ya maoni ya mashauriano. Wapiga kura wa Scotland ambayo ina wakaazi milioni 5.5 walipinga uhuru mwaka wa 2014.

Lakini serikali ya Scotland yenye mamlaka ya ndani inasema kujiondoa kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, ambako kulipingwa na wakaazi wengi wa Scotland, kuna maana kuwa suala hilo linapaswa kupigiwa kura kwa mara ya pili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents