HabariUncategorized

Sehemu ya mahojiano ya Wakili wa Sabaya, Mosses Mahuna na Sahidi wa 10

Kesi ya uhujumu uchumi Na 27/2021 inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya, Lengai Ole Sabaya na wenzake sita inaendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Shahidi namba 10, ambaye ndiyr muathirika katika tukio hilo Francis Mrosso anendelea na kutoa ushahifi wake.

Bongo5.com inakusogeza kuona namna Wakili wa mshtakiwa namba moja(Lengai Ole Sabaya) Wakili Msomi Mosses Mahuna  na Shahidi Mrosso

Wakili : kabla ya kufungua Mrosso Injector Pump service ulikuwa unafanya kazi wapi?

Shahidi: Arusha Delta

Wakili Mwenye Arusha Delta anaitwa Mwamsera

Shahidi: Hilo jina silijui, anaitwa Mamsera

Wakili : Uliondoka kwenye hiyo kazi baada ya kutuhumiwa kuiba vifaa

Shahidi : Si kweli, ningekuwa nimeshafunguliwa mashataka.

Wakili : Gereji yako inajihusisha na magari ya wizi

Shahidi : Si kweli
Wakili: Biashara yako uliifungua kwa kufata taratibu zote

Shahidi : Ndio

Wakili : Katika ufanyaji wako wa biashara umeshawahi kutoa Rushwa?

Shahidi : Kwa kulazimishwa

Wakili: Nijibu ndio/hapana

Shahidi Ndio

Wakili: Hivyo wewe ni mtoa rushwa

Shahidi : Hapana

Wakili : Mtoa rushwa ni mtu wa aina gani?

Shahidi : Mtu anaepindisha sheria

Wakili: Wewe ulitoa nini ili kupindisha Sheria?

Shahidi: Nilitoa rushwa kwa kulazimishwa kutoa fedha.

Wakili: wewe ni mfanya biashara mwaminifu, hujawai kukwepa kodi, kushtakiwa TRA kwanini utoe rushwa?

Shahidi: Rudia swali lako

Wakili : Una matatizo ya kusikia

Shahidi: Nimesema rudia.

Wakili : Anarudia tena.

Shahidi : Nimetoa rushwa kwa kulazimishwa, nilitishwa nitapotezwa au nitapewa kesi ya uhujumu uchumi.

Wakili : Sasa ulitoa fedha ili kuficha nini?

Shahidi: Sina cha kuficha kumbuka waliokuja kwangu ni kina nani!

Wakili: Jibu swali acha story zako za kule gereji
Shahidi : Nakujibu jibu lililopo. Hizo za gereji umeleta wewe

Wakili wa serikali: Mhe. Hakimu Wakili aache kauli za kukera na kumfedhehesha Shahidi.

Wakili : Wewe una imani na Mahakama

Shahidi : Ndio

Wakili : Kwanini hukusubiri upelekwe mahakama ni ili upate haki yako?

Shahidi : Aliyekuja kwangu alikuwa mteule wa Rais, Polisi wilaya ya Hai wapo chini yake. Nikaambiwa nitapotezwa. Alikuja na vijana waliojitambulisha ni Usalama wa Taifa na wengine ni maafisa wa TRA Hata ingekuwa wewe lazima uogope…alinifata pia hadi kwangu. Mtu mwenye familia ukiambiwa utapotezwa lazima uogope.

Wakili: Kwanini hukuripoti polisi hiyo siku ya tarehe 22?

Shahidi : Nilikuwa natafakari..Matukio mengi Mkuu huyo wa wilaya aliyoyafanya na hajachukuliwa hatua.

Wakili : Kwahiyo ulitoa rushwa bila kutafakari?

Shahidi : nisingeweza kutafakari

Wakili : Umewapa rushwa kiasi gani PCCB ili usiunganishwe kwenye kesi hii

Shahidi : Sijatoa rushwa, mimi si mtoa rushwa.

Wakili : Ulitumia simu yako kumpigia kijana anaeitwa Juma ambaye ni bodaboda?

Sahidi : Ndio chini ya ulinzi wao.

Wakili : Ulimpigia mtu anaitwa Mzee Kazibira

Shahidi: Ndio chini ya ulinzi na kwa ruhusa ya vijana niliokuwa nao.

Wakili : Kuna mahali ulisema umepokonywa simu?

Shahidi: sikunyang’anywa simu.

Wakili: umeoa,?

Shahidi : Ndio

Wakili : Simu yako inatuma sms
Shahidi : Ndio

Wakili: Ni kweli hukumtumia mkeo sms kumuambia kama upo chini ya ulinzi?

Shahidi : Sikumtumia

Wakili : Pale Bank kwa mromboo kuna Askari, wenye bunduki lkn pia hukuwaambia kwamba unalazimishwa kutoa fedha?

Shahidi: Sikuweza kuwaambia maana hata askari wapo chini yake Sabaya.

Wakiki: Kwanini hukupiga yowe usaidiwe.

Shahidi: Hata niliokuwa nao walikuwa ni Usalama kama nilivotambulishwa hivyo wangeweza kutoa vitambulisho vyao na nisingeweza kupata msaada.

Mahakama inaendele leo ambapo Sahidi atahojiwa na Wakili fidolin Bwemelo.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents