HabariSiasa

Seneta afukuzwa bungeni Kenya kwa kuvaa suti yenye madoa ya hedhi

Seneta wa Kenya alifukuzwa bungeni baada ya kuhudhuria kikao akiwa amevalia suti nyeupe iliyokuwa na alama rangi nyekundu (kuashiria hedhi) katika kampeni inayoonekana kuwa ya harakati za kushinikiza upatikanani wa taulo za hedhi.

Gloria Orwoba, wa muungano unaotawala, anatarajiwa kuwasilisha hoja kuhusu mswada wa kutoa taulo za bure siku ya Jumatano kama sehemu ya juhudi za kumaliza umaskini wa muda.

Maseneta walitatiza kikao cha Jumanne alasiri ili kumfahamisha spika kwamba Bi Owoba alikuwana “mavazi yasiyofaa”.

Lakini seneta huyo alipinga akisema: “Nashangaa kwamba mtu anaweza kusimama hapa na kusema kwamba bunge limefedheheshwa kwa sababu mwanamke amepata hedhi.”

Spika Amason Kingi aliamuru seneta huyo kwenda kubadilisha nguo zake kabla ya kureruhusiwa tena bungeni.

“Sio kosa kuwa na hedhi… Seneta Gloria nasikitika unapitia hali ya kimaumbili, suti yako imepata madoa ya ajabu, naomba uondoke ili ukabadilishe urudi na. nguo ambazo hazina madoa,” msemaji alisema.

Nje ya ukumbi, Seneta Owoba aliwaambia waandishi wa habari:

Quote Message: Tunalenga kutokomeza janga linalotokana na unyanyapaa wa hedhi. Baadhi ya mambo ambayo ninayotetea na kubuni sheria na kuhakikisha kwamba tunatoa bure taulo za hedhi kwa watoto wote wanaokwenda shule.” from Gloria Orwoba

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents