HabariMichezo

Serengeti Girls waichapa Southampton 3-0

Timu ya taifa ya wasichana U17 Serengeti Girls imefanikiwa kupata ushindi wa goli 3-0 dhidi ya timu ya Southampton ya Ligi Kuu England katika mchezo uliyopigwa Uwanja wa Snows Totton Uingereza.

Huu ni mchezo wa pili wa kirafiki kwa Serengeti Girls nchini Uingereza baada ya ule wa awali dhidi ya timu ya SFC development Squad kumalizika kwa sare tasa ya bila kufungana.

Serengeti Girls U17 ipo Southampton, England kwa kambi ya kujiuandaa na fainali za Kombe la Dunia mwezi Oktoba.

Zikiwa zimebaki siku 11 kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia Oktoba 11, 2022 hadi Oktoba 30, 2022 pale nchini India, timu ya Serengeti Girls U17 imeonyesha ukomavu mkubwa na tayari kuliwakilisha taifa la Tanzania vema.

Tanzania imepangwa kundi D kwenye michuano hiyo ya FIFA kwa upande wa wanawake walio na umri chini ya miaka 17 (U17) ambapo kuna timu za Japan, Ufaransa na Canada.

Imeandikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents