Habari

Serikali kuja na mwarobaini wadanganyifu wa mitihani

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema inafanya mapitio ya sheria ya Elimu ili kuhakikisha adhabu kali zinatolewa kwa wanaoshiriki kufanya vitendo vya udanganyifu katika Mitihani ya Kitaifa.
Muarobaini 

Hayo yamesemwa na Waziri wa wizara hiyo Prof. Adolf Mkenda, Jijini Dar es Salaam ambapo amesema wanaongea na mamlaka husika ili wanaovujisha na kufanya vitendo vya udanganyifu katika mitihani wasiishie kufukuzwa kazi tu bali wachukuliwe hatua za kisheria kwa kuwa vitendo hivyo ni vya jinai.

Ameongeza kuwa imebainika udanganyifu mara nyingi hufanyika katika vituo vya kufanyia mitihani ambapo watumishi wasio waaminifu hushiriki katika njama hizo ambazo hazina tofauti na uhujumu uchumi.

“kuna hata watumishi wa umma ambao wanashiriki katika udanganyifu, nisisitize kwamba unapotaka kuua taifa basi chezea elimu, nasi hatutakubali kuona taifa linaharibiwa na watu wachache wasio waaminifu,” amesisitiza waziri.

Amesema udanganyifu katika mitihani una madhara ya kumwezesha mtu ambaye hakustahili kuendelea na masomo kuendelea na mwisho kupatikana mtaalamu asiye na viwango.

Prof. Mkenda amesema Baraza la Mitihani la Tanzania limeongeza Mikakati ya kupambana na watu ambao wanafanya udanganyifu kwenye mitihani, aidha kubaini shule mbalimbali ambazo wasimamizi pamoja na walimu wameshirikiana kwa namna moja au nyingine kufanya udanganyifu huo.

Ameongeza Serikali kuwepo katika mapitio ya sera na mabadiliko ya mitaala haimanishi imesimamisha jukumu la kusimamia utoaji elimu hivi sasa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents