Habari

Serikali kutoa vifaa vya kisasa kwa Jeshi la Zimamoto

SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inatarajia kutoa vifaa vya kutosha na vya kisasa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kupunguza mazingira hatarishi kwa askari pindi wanapotekeleza majukumu yao hasa ya majanga ya moto.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni Wakazi alipowatembelea askari wawili wa Jeshi hilo la Zimamoto a Uokoaji ambao waliungua na moto wakati wakitekeleza majukumu yao ya ukoaji wa watu kwenye ajali ya gari iliyotokea Maci 28, 2024 eneo ya Mlandizi mkoani Pwani.

Askari hao ambao ni 3463 Koplo Hamisi Kungwi ambaye yupo Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) na 3384 Koplo Elias Bwire yupo wodi ya kawaida wapo katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam wakiendelea kupatiwa matibabu.

Waziri Masauni amesema askari wanapotekeleza majukumu yao hasa ya kuokoa maisha ya watu na mali zao wakati mwingine wanafanyakazi hiyo katika mazingira hatarishi hivyo serikali itatoa vofaa hivyo ili kuboresha mazingira yao ya ufanyaji kazi.

“Askari wanapokuwa na vifaa vya kisasa ile hatari ya wao kupata madhara pindi wanapotekeleza majukumu yao inapungua .
Serikali inaendelea kufanya kazi kubwa sana hasa kuhakikisha mazingira ya askari katika kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao ikiwemo mutukio ya moto yanakuwa mazuri zaidi,” amesema

Waziri Masauni amesema askari wanapotekeleza majukumu yao hasa ya kuokoa maisha ya watu na mali zao wakati mwingine wanafanyakazi hiyo katika mazingira hatarishi hivyo serikali itatoa vofaa hivyo ili kuboresha mazingira yao ya ufanyaji kazi.

“Askari wanapokuwa na vifaa vya kisasa ile hatari ya wao kupata madhara pindi wanapotekeleza majukumu yao inapungua .
Serikali inaendelea kufanya kazi kubwa sana hasa kuhakikisha mazingira ya askari katika kutekeleza majukumu yao ya kulinda usalama wa raia na mali zao ikiwemo mutukio ya moto yanakuwa mazuri zaidi,” amesema

Aidha amesema amefika katika hospitali hiyo ya Mloganzila kwa lengo la kuwajulia hali askari hao ambao amekuwa akifuatilia taarifa zao kwa ukaribu tangu waliookolewa na kulazwa katika hospitali hiyo.

Kwa upande wa askari ambaye amèlazwa hospitali hapo, Koplo Bwire amesema anamshukuru Waziri na serikali kwa ujumla kwa kuweza kuwajulia hali na kuwapa mkono wa pole.

“Hii ni ajali kama zilivyoajali nyingine, ni kweli tumepata ajali tukiwa kazini lakini tunashukuru kwa namna ambavyo tumepata huduma, nakushukuru sana Waziri wa kufika hospitali hapa na kutujulia hali Mungu akubariki sana,” amesema Bwire

Ajali iliyosababisha askari hao kujeruhiwa ilitokea Machi 28 mwaka huu saa 10:15 alfajiri katika bonde la Ruvu Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani barabara ya Morogoro, Dar es Salaam.

Inaelezwa kuwa gari namba T668 DTF aina ya Scania Kampuni ya Sauli ikiendeshwa na dereva Idd Aloyce (35), mkazi wa Mafinga ikitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya liligonga ubavuni lori la mafuta ya Petroli lenye namba za usajiri RAF672N na tela lenye namban RL2594 aina ya Howo lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda nchini Rwanda likiendeshwa na dereva Mushimana Musiyimana lililokuwa limesimama kupisha gari lililokuwa linakuja mbele yake.

Aidha basi hilo lilikuwa limeongozana na basi la Golden Deer Kampuni ya New Force lenye namba za usajiri RAF672N na likiendeshwa na dereva aitwaye Burton Jacob (33),.mkazi wa Mbeya ambapo nalo lililigonga kwa nyuma basi la Saul lililokuwa mbele yake na kusababisha vifo vya watu wawili ambao hawakufahamika majina yao na majeruhi watatu ambao ni Salimu Daud (50) mkazi wa Mbozi Mbeya, Farida Idrisa (26)mkazi wa Tabata Dar es Salaam na Kiambile Geofrey mkazi wa Uyole Mbeya.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents