Habari

Serikali kuwafikisha mahakamani waliomshambulia Tundu Lissu

Waziri Simbachawene ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, na kusisitiza kwamba Jeshi la polisi linazo kesi nyingi za aina hiyo hivyo haliwezi kufanya upelelezi maalum kwa ajili ya mtu mmoja.

Aicha Waziri Simbachawene ameongeza kwamba mpaka sasa wapo wahusika waliokamatwa katika upelelezi na wengine wameshindwa kupatikana kwa kuwa namna ya kuwapata imekua ni ngumu.

“Tuna kesi nyingi sana, hiyo kesi unayoisema ambayo sitaki hata kuitaja ni miongoni mwa kesi tunazozipeleleza, hatuwezi kuwa na specialization kwa ajili ya kesi ya mtu mmoja tunapeleleza kwa mujibu wa sheria na tutachukua hatua kwa mujibu wa sheria, hivyo upelelezi na uchunguzi unaendelea pale ambapo tutakuja kuwapata wahusika tutawafikisha mahakamani,” amesema Waziri Smbachawene.

Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi Septemba 07, 2017 nje ya makazi yake huko Jijini Dodoma, alipokuwa akirejea nyumbani kwa ajili ya chakula cha mchana baada ya vikao vya Bunge vya siku hiyo.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents