HabariSiasa

Serikali yafuta tozo kuhamisha fedha benki-simu

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, leo amewasilisha kauli ya Serikali kuhusu Tozo, Mhe. Dkt. Mwigulu amesema itakumbukwa kuwa katika mwaka wa fedha 2021/22, Sheria ya Malipo ya Taifa, Sura na. 437 (National Payment System Act, Cap. 437) ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na kuanzisha tozo ya miamala ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu za mikononi yaani, Mobile Money Transaction Levy. Sambamba na tozo hii, tulipandisha tozo kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha mfuko wa TARURA na Mfuko wa Elimu ya juu.

Waziri wa Fedha, anasema lengo la kuanzisha tozo hizo ni kuunganisha nguvu na umoja wa Watanzania wote katika kuiwezesha Serikali kuongeza kasi ya kutekeleza miradi hasa ile iliyokosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti ili kuwakwamua Wananchi dhidi ya ukosefu wa huduma za jamii-msingi kwa kuzingatia kuwa sura ya bejeti yetu karibu kila mahitaji ni mahitaji ya lazima, marekebisho yatakayofanyika ni kama ifuatavyo;
a) Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote);

b) Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote);

c) Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote).

 

Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote), Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote), Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote).

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents