Habari

Serikali yaipongeza Vodacom kwenda sambamba na kasi ya kuhamia Dodoma

Naibu Waziri wa Kazi Vijana na Ajira,Mh.Antony Mavunde, ameipongeza kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Plc kwa kuzidi kuimarisha huduma zake mkoani Dodoma hususani kipindi hiki ambacho Serikali imehamishia makao yake mkoani humo na ofisi nyingi za serikali zikiwa zinazidi kuhamia.


Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira,Vijana na wenye ulemavu Antony Mavunde(katikati)akikata utepe kuashiria Uzinduzi rasmi wa duka jipya la VodacomTanzania Plc lililopo eneo la Kizota mjini Dodoma ,kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa kampuni hiyo ,Jacqueline Maturu na kushoto ni Mkuu wa maduka ya rejareja na mauzo wa kampuni hiyo, Brigita Stephen

Akizindua duka jipya na la kisasa la kampuni hiyo eneo la Kizota mwishoni mwa wiki,Mh.Mavunde alisema kuwa serikali inatambua kuwa sekta ya mawasiliano inachochea maendeleo ya nchi haraka ndio maana imekuwa ikifanya jitihada za kuboresha mazingira ya uwekezaji katika sekta hii ili kuwezesha wawekezaji kusambaza huduma za mawasiliano nchini kote,maeneo ya mijini na vijijini.

“Nawapongeza Vodacom kwa kuongeza nguvu ya huduma zenu kwa kufungua duka jipya mbali na maduka yaliyopo,hatua hii inadhihirisha kuwa mnaenda sambamba na kasi ya serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambapo tayari shughuli nyingi za serikali zinafanyika mjini hapa na idadi ya wakazi inaongezeka hivyo mawasiliano bora yanatakiwa,” alisema.

Aliwataka wakazi wa Dodoma kuchangamkia fursa mbalimbali zinazojitokeza kama vile kutembelea duka hili jipya la Vodacom kwa aili ya kupata huduma za mawasilaino ikiwemo kujua huduma za kubadilisha maisha ya wananchi zinazotolewa na kampuni ya Vodacom bila kusahau kujitokeza kununua hisa zake katika mchakato wa kuuza hisa unaoendelea.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo, Jacquiline Materu,alisema Vodacom itaendelea kutekeleza dhamira yake ya kurahisisha mawasiliano na kufanya ubunifu wa kiteknlojia kupitia mtandao wake lengo kubwa likiwa ni kuwapeleka watanzania katika ulimwengu wa kidijitali.

“Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko mengi kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Vodacom imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika”.Materu

Kampuni ya Vodacom ambayo ni ya kwanza kuanza mchakato wa kuuza hisa zake katika sekta ya mawasiliano nchini imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents