Habari

Serikali yatangaza Sensa

Serikali imewataka wananchi kujiandaa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano katika zoezi la hesabu ya watu na makazi (Sensa) inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.

“Niwakumbuushe Watanzania mwakani mwezi wa nane tutakuwa na zoezi la kuhesabina kujua tupo wangapi, tutatangaza tarehe rasmi, kila mmoja aikumbuke na ajitokeze ili itusaidie kupanga mipango ya maendeleo. Kila mmoja awe tayari mwakani kwa tarehe itakayopangwa,” amesema.

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo Sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012.

Hivyo Sensa ya mwaka 2022 itakuwa ni sensa ya Sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964, Sensa zingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

BY : Fatuma Muna

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents