Habari

Serikali yaweka wazi namba na e-mail za waganga wakuu kila mkoa

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetoa mawasiliano ya waganga wakuu wa kila mkoa kuwarahisishia wananchi wanaotaka kutuma malalamiko na kero zao. Chini ni taarifa zaidi.

Coat_of_arms_of_Tanzania.svg

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya.

Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007). Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika kupata huduma za afya.

Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: [email protected]

“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.

MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)

MKOA
JINA LA MGANGA MKUU
NAMBA YA SIMU
NUKUSHI
1.
ARUSHA
DKT. FRIDA MOKITI
0784-264750
[email protected].
2.
DAR ES SALAAM
DKT. GRACE MAGEMBE
0767-300234
[email protected]
3.
DODOMA
DKT. JAMES CHALRES
0784-504955
[email protected]
4.
IRINGA
DKT. ROBERT M. SALIM
0754-377176
[email protected]
5.
KAGERA
DKT. THOMAS RUTACHUNZIBWA
0754-803729
[email protected]
6.
KIGOMA
DKT. PAUL CHAOTE
0755-696855
[email protected]
7.
KILIMANJARO
DKT. BEST MAGOMA
0754-621046

8.
LINDI
DKT. SONDA YUSUPH
0653-384350
[email protected]
9.
MANYARA
DKT. SUNGWA KABISSI NDAGABWENE
0713-450765
[email protected]
10.
MARA
DKT. SAMSON WINANI
0784-450425
[email protected]
11.
MBEYA
DKT. SEIF MHINA
0767-832275
[email protected]
12.
MOROGORO
DKT. JACOB FRANK
0767-985850

13.
MTWARA
DKT. WEDSON SICHALWE
0755-048787

14.
MWANZA
DKT. LEONARD SUBI
0784-501020
[email protected]
15.
PWANI
DKT. BEATRICE BYARUGABA
0784-319764
[email protected]
16.
RUKWA
DKT. JOHN GURISHA
0784-216008
[email protected]
17.
RUVUMA
DKT. DAMAS KAYERA
0713-537495
[email protected]
18.
SHINYANGA
DKT. NTULI KAPOLOGWE
0654-586346
[email protected]
19.
SIMIYU
DKT. MAGEDA KIHULYA
0754-507875
[email protected]
20.
SINGIDA
DKT. JOHN MWOMBEKI
0786-103225
[email protected]
21.
TABORA
DKT. GUNINI KAMBA
0783-344079
[email protected]
22.
TANGA
DKT. ASHA MAHITA
0715-465521
[email protected]
23.
GEITA
DKT. JOSEPH KISALA
0788-046787
[email protected]
24.
KATAVI
DKT. YAHYA HUSSEIN
0754-372772
hyahaya70yahoo.com
25.
NJOMBE
DKT. SAMUEL MGEMA
0757-226806
[email protected]

IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents