FahamuHabariTechnology

Setilaiti ya kwanza ya Kenya Taifa-1 yarushwa angani baada ya majaribio matatu

Taifa-1, setilaiti ya kwanza ya Kenya ya kufuatilia dunia, imerushwa angani kwa roketi ya SpaceX Falcon 9 kutoka kituo cha Anga cha Vandenberg huko California, Marekani.

Space-X ambayo makao yake makuu ni nchini Marekani, na hutengeneza na kurusha roketi za kisasa zaidi kwenye anga za juu zaidi duniani, awali ilikuwa imeghairi kuinua roketi ya Falcon 9 mara tatu kutokana na hali mbaya ya hewa.

Uzinduzi wa awali ulipangwa kuafnyika Jumatatu lakini ulicheleweshwa kwa saa 24 hadi Jumanne kutokana na hali mbaya ya hewa.

Siku ya Jumanne, misheni hiyo ilicheleweshwa kwa mara nyingine tena hadi Ijumaa 9:48 saa za Afrika Mashariki kwa matumaini kwamba kufikia wakati huo kungekuwa na hali ya hewa iliyo imara.

Uzinduzi huo ukaahirishwa tena kwa saa 24 hadi Jumamosi asubuhi 9:48 EAT baada ya roketi kuachiliwa angani na takriban dakika tisa baadaye, ikarejea duniani ikigusa eneo la kutua la 4 la Space X.

Satellite ya Taifa-1 ya Kenya itatumika kukusanya takwimu za ufuatiliaji wa kilimo, ardhi na mazingira.

Satelaiti hiyo itakuwa ya 50 kutumwa na mataifa ya Afrika.

Kufikia sasa, nchi 14 barani humo zimetuma satelaiti angani, huku nyingi zikichagua kampuni za kibiashara kama SpaceX kwa urushaji huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents