HabariMichezo

Shabiki afungiwa miaka 40 kutoingia uwanjani 

Kijana wa miaka 20, shabiki wa Klabu ya PSV Eindhoven amefungiwa miaka 40 kuingia uwanja wa Philips baada ya kumshambulia golikipa wa Sevilla, Marko Dmitrovic wakati wa mchezo wa Europa League.

Shabiki huyo ambaye tayari alikuwa akitumikia adhabu ya miezi mitatu kutoingia uwanjani hapo kabla ya tukio hilo, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka wa Umma imepiga marufuku kukaribia eneo la Uwanja wa Philips kwa miaka miwili.

Kutokana na kutumikia adhabu ya hapo awali alishindwa kununua tiketi na hivyo kununuliwa kupitia jina la rafiki yake.

PSV wanatarajia kupigwa faini baada ya Uefa kuwafungulia kesi ya kinidhamu kufuatia tukio hilo.

Imeadikwa na @fumo255

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents