BurudaniHabari

Shakira kupandishwa kizimbani kwa udanganyifu wa kodi

Mahakama moja katka mji wa Barcelona nchini Uhispania imeamuru nyota wa muziki wa pop duniani, Shakira, kupandishwa kizimbani kukabiliana na mashitaka ya udanganyifu wa kodi inayokisiwa kufikia euro milioni 14 na nusu.

Mahakama hiyo imeamua kuwa kesi hiyo inapaswa kufanyika, hata baada ya mwanamuziki huyo kulipa kiwango kilichodaiwa na Mamlaka ya Kodi ya Uhispania, pamoja na riba ya euro milioni tatu.

Mwezi Julai, waendesha mashitaka walisema wangeliiomba mahakama imuhukumu mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 45 kifungo cha miaka minane jela.

Shakira anatuhumiwa kudanganya kwamba haishi Uhispania, wakati alikuwa akiishi huko pamoja na mshirika wake, mcheza soka Gerard Pique. Wawili hao, ambao wamezaa watoto wawili, walitangaza kutengana mwezi Juni.

Related Articles

Back to top button