Habari

Shambulio shuleni Texas, watu 21 wauawa wanafunzi 19, Rais Biden atoa kauli

Watoto wadogo kumi na tisa na watu wazima wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi katika shule ya msingi kusini mwa Texas baada ya mtu mwenye silaha kufyatua risasi katika Shule ya Msingi ya Robb katika jiji la Uvalde kabla ya kuuawa na vyombo vya sheria, maafisa walisema.

Mbali na kuuawa kwa watoto wadogo kumi na tisa, watu wazima wawili wameuawa akiwemo mwalimu

Mwalimu aliyefariki alikuwa nani?

ggg

Mireles, mwalimu ambaye aliripotiwa kuuawa, alikuwa na umri wa miaka 40 na alikuwa na binti chuoni, kulingana na ukurasa wake kwenye tovuti ya shule.

Alikuwa mwalimu kwa miaka 17. Ukurasa huo ulimnukuu akisema: “Ninapenda kukimbia, kupanda milima, na sasa unaweza kuniona nikiendesha baiskeli!!”

Shangazi yake, Lydia Martinez Delgado, aliambia New York Times mpwa wake “alipendwa sana” na “alikuwa mtu wa kufurahisha katika sherehe”.

Watu Mashughuli na viongozi walioguswa

Maafisa wa Marekani, Maseneti na Wamarekani wengine mashuhuri wameonesha kuguswa na shambulio hilo katika shule ya msingi kusini mwa Texas. na hapa tunawaangazia kauli za baadhi yao.

Rais wa Marekani Joe Biden

ggg

“Nilitarajia nitakapokuwa rais nisingelazimika kufanya hivi tena,” Biden alisema, akilaani vifo vya “watoto wasio na hatia” wa darasa la pili, la tatu na la nne katika “mauaji mengine Marekani.”

Wazazi wao “hawatawaona tena watoto wao, kamwe hawatakuwa anao wakiruka kitandani na kubembelezwa nao,” alisema.

“Kama taifa, inatubidi kuuliza, ‘Ni wakati gani katika jina la Mungu tutaacha kupigia watu risasi?’

“Lazima tuchukue hatua,” alisema na kupendekeza kurejeshwa kwa marufuku ya kutumia silaha na “sheria zingine za zakawaida.”

Mke wa rais wa Marekani Jill Biden

“Mungu, inatosha. Watoto wadogo na walimu wao.

kupigwa na butwaa. hasira. kuvunjika moyo.”

Seneta wa Democratic Chris Murphy

“Niepushe na uwongo kuhusu ugonjwa wa akili… Hatuna ugonjwa wowote wa akili kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Huwezi kuelezea hili kupitia ugonjwa wa akili kwa sababu sisi sio watu wa kipekee na magonjwa ya akili. . .. Sisi ni wa kipekee linapokuja suala la upatikanaji wa silaha na uwezo wa wahalifu na watu wagonjwa sana kupata silaha. Hilo ndilo linaloifanya Amerika kuwa tofauti.”

Seneta wa Utah Republican Mitt Romney

“Huzuni huijaza roho. Watoto wakichinjwa. Maisha yamezimwa. Mioyo ya wazazi inauma. Natuma salamu za rambirambi lakini najua haitoshi kabisa. Lazima tupate majibu.”

Seneta wa West Viginia Joe Manchin

“Hiyo haina maana hata kidogo, kwa nini hatuwezi kufanya mambo ya kawaida, ya kawaida na kujaribu kuzuia baadhi ya haya kutokea.

Rais wa zamani Barack Obama

ggg

“Takriban miaka kumi baada ya Sandy Hook na siku kumi baada ya mauaji ya Buffalo, nchi yetu inapooza, si kwa hofu, lakini kwa ushawishi wa bunduki na chama cha kisiasa ambacho hakijaonyesha nia ya kuchukua hatua yoyote ambayo inaweza kusaidia kuzuia majanga haya. Ni muda mrefu umepita wa kuchukua hatua, aina yoyote ya hatua. Na ni janga lingine .”

Makamu wa rais Kamala Harris

ggg

“Inatosha … Kama taifa, tunapaswa kuwa na ujasiri wa kuchukua hatua na … ili kuhakikisha jambo kama hili halitokei tena.”

Rais wa zamani Bill Clinton

“Viongozi wetu waliochaguliwa katika ngazi za mitaa, majimbo na ngazi za shirikisho, bila kujali vyama, lazima watafute njia za busara za kuwaweka watoto wetu na jamii salama. Wanaweza kufanya hivyo bila kugusa haki ya kuwinda, kufyatua risasi na kushika bunduki kwa ajili yao wenyewe. -Utetezi. Propaganda zimetuzuia kusaidiana kwa hili kwa muda mrefu sana. Tunaweza kufanya – na kuwa – bora zaidi. Wakati wa kuchukua hatua ni sasa.”

Mshukiwa wa tukio hili ambaye alikuwa na bunduki aina ya AR-15 semiautomatic pia anashukiwa kumuua bibi yake kabla ya kufanya tukio la kufyatua risasi shuleni, vyanzo vitatu vya sheria vilithibitisha kwa CBS News, mshirika wa BBC Marekani.

Mashambulizi ya silaha yameongoza na kusababisha vifo nchini Marekani kuliko ajali za gari kwa mwaka 2020, kulingana na data iliyotolewa na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) mwezi uliopita.

Kuna bunduki ngapi Marekani?

ddd

Bunduki ni suala la kisiasa sana nchini Marekani – likiwahusisha watetezi wa udhibiti wa bunduki dhidi ya wale wanaolinda vikali haki yao ya kikatiba ya kubeba silaha.Hivi karibuni tukio la mtoto mwenye umri wa miaka 18 ambaye alidaiwa kushambulia duka la mboga huko Buffalo, New York, tarehe 14 Mei ambapo pia alikuwa amevalia silaha za mwili na kubeba bunduki ya nusu-otomatiki – zote zinapatikana kwa kununuliwa nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents