HabariSiasa

Sheria ya umiliki wa silaha Marekani yachukua sura mpya

Wabunge wa Marekani wamezindua muswada wa sheria ya kushughulika janga la uhalifu wa bunduki lililoligubika taifa hilo. Ikipitishwa itasaidia kudhibiti umiliki wa bunduki na kukabiliana na ogezekola uhalifu wa bunduki.

Wabunge hao kutoka vyama vyote viwili vya Republican na Democrat wameelezea imani yao kwamba sheria hiyo itapitishwa na itasaidia pakubwa kudhibiti umiliki wa bunduki na hatimaye kukabiliana na ogezeko la matukio ya mashambulizi ya bunduki yanayoibua hofu kubwa nchini Marekani.

Wabunge hao amesema wana uhakika kwamba sheria hiyo itaungwa mkono na pande zote mbili na huenda ikamfikia rais Joe Biden wiki ijayo.

Kiongozi wa maseneta wa chama cha Democrat Chuck Schumer amenukuliwa akisema sheria hiyo ya usalama wa bunduki ni hatua kubwa na itasaidia kuokoa maisha. Amesema ingawa haijajumuisha kila kiu wanachokihitaji, lakini inahitajika kwa dharura.

Kundi hilo la wabunge lilikubaliana kuhusu mfumo ambao utajumuisha uchunguzi wa kina historia ya wanunuzi walio na umri wa chini ya miaka 21 na ufadhili wa afya ya akili pamoja na programu za usalama shuleni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents