Shetta: Ntamsaidia Diamond kwenye taasisi yangu, amefanyiwa ukatili kufichwa baba yake (+ Video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na Mkurugenzi wa Taasisi ya kusaidia ukatili katika jamii ya Sawa, Nurdin Bilal Ali alimaarufu  Shetta amezungumzia sakata la msanii mwenzake Naseeb Abdul alimaarufu Diamond Platnumz kumfichwa baba yake mzazi hadi umri huu alionao.

Shetta ameongeza kuwa ukatili kwa binadamu yeyote sio lazima uwe wa kijinsia bali kuna ukatili wa aina nyingi mfano ukatili wa kihisia ambao umejitokeza kwenye sakata la Diamond na wazazi wake.

Kuhusu Diamond kumfichwa baba yake mzazi mpaka hivi sasa anaweza kwenda mahakamani kudai haki yake kama mtoto na baada ya kwenda kushtaki sisi kama Taasisi ya Sawa kwa kutumia wanasheria wetu tutaanza kumsaidia.

Lakini pia mzazi (Baba) kukataa mtoto kutumia jina lake hilo limekaa kisheria zaidi ambapo mzazi anaweza kwenda mahakamani kushtaki na baada ya hapo sisi kama Taasisi kupitia wanasheria wetu tutaanza kushughulika nalo.

Related Articles

Back to top button
Close