Shirikiana na uliyeshirikiana nae kumleta mtoto- Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewataka wanaume kuacha kukimbia majukumu ya ulezi na kutekelezea wanawake peke yao.

Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia ameyasema hayo leo 6, Oktoba katika sherehe za uzinduzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, huko Jijini Dodoma.
Amesisitizia hayo wakati akiwapongeza viongozi wa Mahakama kuanzisha kituo maalumu cha kushughulikia mambo ya kifamilia yakiwemo, mirathi, ndoa talaka, malezi na matunzo ya watoto kwenye Kituo cha Utoaji Haki katika Wilaya ya Temeke, kwani Wanawake na watoto wamekuwa wakiteseka.

Mmefikiri vema kutowajibika kwa wanaume, mmeamua kutenga vyumba maalumu kwa shughuli zao. Hii ikawakumbushe wanaume kuwajibika. Umeleta kiumbe duniani wajibika. Umeacha mtoto mahala wajibika. Usijifiche huyo kiumbe ulikileta pasipo yeye kutaka. Shirikiana na uliyeshirikiana nae kumleta duniani ili kumtunza,” amesema.

BY: Fatuma Muna

 

Related Articles

Back to top button