BurudaniHabari

Show za Diamond nyingi anaenda zaidi Babu Tale na sio Sallam Sk kama zamani, unahisi kwanini??

Kupitia kwenye kipindi chake pendwa cha RECAP & MANDO @el_mando_tz amezungumiza kuhusu namna Uongozi wa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ulivyo kwa sasa.

@el_mando_tz anatusanua kuwa kwa sasa Babu Tale ndio amekuwa meneja ambaye yupo karibu zaidi na Diamond akifuatiwa na Mkubwa Fella lakini meneja wa Diamond wa tatu ambaye ni Sallam Sk amekuwa haonekani zaidi na Diamond.

Anaongeza kuwa mara ya mwisho Sallam Sk kuonekana na Diamond ilikuwa Zanzibar baada ya show ya Diamond ya Mtwara kushindwa kumalizika na baada ya hapo hajaonekana tena akiwa na Diamond.

Ukirudi nyuma kidogo show ya Diamond ya Uganda Sallam Sk alikuwepo lakini zingine Sallam Sk hajaonekana kabisa kwenye show za Diamonb na mara zote amekuwa akionekana Babu Tale.

@el_mando_tz anahoji kuwa huenda kuna utofauti kati ya Diamond na Sallam Sk?? kwa sababu sio kawaida yake na mara nyingi alikuwa akishiriki hata kwenye Tamasha la Diamond na Wasafi Festival.

Awamu hii Sallam Sk hajaonekana wala hajapost Tamasha la Msanii wake.

Kama hawana utofauti unahisi ufanyaji kazi wa Sallam kwa sasa upoje na Diamond?? maana hata matamasha na show za nje haendi sana kama Babu Tale??

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents