BurudaniHabari

Shu ya Diamond ndio Amapiano bora Tz?? vipi kuhusu Single Again na Sumu??

Kupitia kwenye kipindi cha RECAP & MANDO @el_mando_tz ameizungumzia kauli ya Diamond ya kusema ngoma yake ya AMAPIANO ya SHU ndio bora zaidi Tanzania.

@el_mando_tz kwa upande wake ametaja nyimbo mbili ambazo anahisi ni bora kuliko SHU na ametaja sababu zake kadhaa ambazo zinafanya nyimbo hizo ziwe bora kuliko SHU.

Moja ya sababu aliyoitaja ni takwimu ambazo ameangalia zaidi Youtube pia Boomplay na Spotify Single ya Harmonize inaongoza kwa takwimu ikifuatiwa na SHU ya Diamond.

Sababu nyinginne aliyoitaja ni ujumbe au meseji iliyopo kwenye SHU pamoja na Single Again ya Harmonize na SUMU ya Alikiba Ft Marioo, kwenye upande wa Ujumbe @el_mando_tz anasema Single Again na Sumu zina ujumbe mkubwa na mzuri kuliko Shu.

Anasema kuwa wimbo huo wa Shu umefanya vizuri zaidi TikTok maana watu wameutumia kwenye challenge nyingi lakini ukija mtaani na kwenye sehemu nyingi za kusikiliza muziki Single Again na Sumu zimechezwa zaidi na pia jumbe zao au meseji zinafanya nyimbo hizo zisikilizwe zaidi na kupendwa zaidi.

Kwako wewe unanhisi Amapiano ipi kali Tanzania??

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents