Habari

SIDO kuendelea kuwasaidia wajasiriamali kuanzisha viwanda vidogo vidogo

SHIRIKA la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limeendelea kuhakikisha linawasaidia wananchi na wajasiriamali kuanzisha, kuendeleza na kuimarisha misingi ya ubunifu kwa lengo la kuongeza fursa za ajira.

Akizungumza jijini Dar es salaam kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya kimataifa maarufu Sabasaba yanayoendelea, Mkurugenzi Mkuu SIDO, Sylvester Mpanduji amesema kupitia huduma wanazozitoa kuna wajasiriamali ambao wamefaidika kwa kupata mikopo ambayo imesawadia kuanzisha viwanda vyao.

Aidha Mpanduji amesema katika Maonesho hayo wameingia na teknolojia ya majiko ya nishati safi ya kupikia ambapo kwa watu watakaotembelea banda lao watapata nafasi ya kununua kwa ajili ya matumizi yao.

Mpanduji ameeleza kuwa changamoto ya kubangua korosho moja moja sasa suluhisho lake llimepatikana kwa kuundwa mtambo wa teknolojia ya kisasa ambao wanavikundi au mtu mmoja mmoja akitumia itasaidia kuchochea ongezeko la viwanda vidogo.

Written by Janeth Jovin

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents