
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amedai hajashtushwa na taarifa za Klabu hiyo kuachana na Cristiano Ronaldo huku akiamini kuwa hakukuwa na chaguo lingine dhidi ya kumuacha staa huyo aondoke.
‘’Kushtushwa ? Hapana,’’ Amekiambia chombo cha habari Sport 18, kupitia Sun.
‘’Hakukua na chaguo lingine, lakini ni haibu kwasababu ni mtumishi mzuri ndani ya klabu.’
‘’Namtakia kila lakheri popote aendapo.’’
United imetangaza kuachana na Ronaldo usiku wa siku ya Jumanne baada ya mahojiano yake na Piers Morgan yaliokuwa yakiukoso uongozi wa timu, Kocha wake na Rooney.
Uongozi wa timu hiyo ilitoa taarifa yenye jumla ya maneno 67 yalioeleza kuachana na Ronaldo aliyesalia miezi saba pekee kwenye kandarasi yake huku akivuta paundi 500,000 kwa wiki.