Sikurudi Man United kuwania ‘Top Four’, wala kucheza Europa League – Ronaldo 

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Cristiano Ronaldo amesema kuwa wananapaswa kupambana kuhakikisha timu hiyo inakuwa ndani ya tatu bora ya msimamo wa ligi mwisho wa msimu na kusisitiza kutokuwa kwenye nafasi hiyo kutakuwa ni kufeli.

Man United fans want Cristiano Ronaldo to be captain after his rousing Sky Sports interview

Ronaldo amesema kuwa hajaondoka Juventus kuja kupambania nafasi ya nne ”Manchester United inapaswa kutwaa ubingwa wa Ligi, kushika nafasi ya pili au ya tatu.”

”Sioni nafasi nyingine kwa Manchester United kuwa mkweli sioni nafasi nyingine. Sitaweza kukubali uwezo wetu kubaki nje ya tatu bora kwenye Premier League.”

Ronaldo gave his back to interim boss Ralf Rangnick but insisted there must be changes

Ronaldo anaamini kuwa anaamini wanayonafasi ya kuwania ubingwa tangu alivyorejea Old Trafford kipindi cha majira ya joto kilichopita, lakini hata hivyo United tayari imezidiwa jumla ya point  22 kutoka kwa vinara wa Ligi Manchester City huku wakishika nafasi ya saba (7).

Mchezaji huyo mwenye mafanikio makubwa kunako mchezo wa mpira wa miguu, Ronaldo ambaye mpaka sasa ameshafunga magoli 14 kwenye michezo 21 amesema kuwa kocha wake Mjerumani Ralf Rangnick anafanya vizuri isipokuwa anahitaji apewe muda.

IMEANDIKWA NA @fumo255

Related Articles

Back to top button