Habari

Silaha haramu 6,000 zateketezwa Dar

Naibu Waziri wa Mambo ya ndani nchini, Jumanne Sagini ameliagiza Jeshi la polisi kufanya uchunguzi kwenye mikoa iliyoongoza kwa usalimishaji wa silaha haramu, ili kubaini vyanzo na matumizi ya silaha hizo.

Kwa mujibu wa Eatv. tv. Silaha zaidi ya elfu sita zimeteketezwa leo katika uwanja wa Jeshi wa Shabaha Kunduchi Dar es Salaam ambapo kati ya hizo zipo silaha 1220 zilizosalimishwa katika kampeni ya usalimishaji wa silaha haramu kwa hiari, zoezi lililofanyika kuanzia Sep 1 hadi Oktoba 31 mwaka huu na mikoa ya Tanga, Tabora na Pwani imeongozwa kwa usalimishaji.

Aidha Naibu Waziri Sagini amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kudhibiti vitendo vya uharifu vinavyofanya na vikundi kama panya road, katika mikoa mingine baada ya vikundi hivyo kudhibitiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Kwa upande wake Kamishina wa Oparesheni na Mafunzo ya Polisi nchini, (CP) Liberatus Sabasi am
akafafanua zaidi kuhusu silaha zilizoteketezwa huku akisisitiza zoezi hili limefanyika hadharani ili wananchi washuhudie.

Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Kheri James, amewataka ndugu wa watu waliofariki dunia, waliokuwa wakimiliki silaha kihalali, kuzisalimisha silaha hizo kwa jeshi la Polisi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents