HabariMichezo

Silva akataa kufuata nyayo za Ronaldo

Kiungo Mshambuliaji, David Silva amekataa kujiunga na Saudi Pro League licha ya ofa nyingi kumiminika mezani kwake kutoka kwa mawakala wa Saudi Arabia wakionesha nia ya kutaka huduma yake.

Staa huyo wa Hispania, Silva hana mpango wa kufuata nyayo za Cristiano Ronaldo ambaye mwezi Desemba, 2022 alifungua njia kwa wachezaji wengine wenye majina makubwa Barani Ulaya kutaka kujiunga na Ligi hiyo inayozungumzwa mno mitandaoni tangu kusajiliwa kwake.

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City bado anahitaji kuwa na familia yake Hispania wakati huu ambao anaitumikia Klabu ya Real Sociedad.

Ronaldo kujiunga na Klabu ya Al- Nassr ya Saudi Arabia kulizua gumzo ulimwengu mzima na sasa nchi hiyo iaangazia wachezaji wengine wenye majina makubwa ambao watasajiliwa huku David Silva akiwa ni miongoni mwao.

Imeandikwa na @fumo255

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents