Michezo

Simba Bingwa wa Mapinduzi Cup 2022

Simba SC wamefanikiwa kutwaa Ubingwa wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Azam FC goli 1 – 0.

Bao pekee la penati la Meddie Kagere dakika ya 56 ya kipindi cha pili ndiyo limepatia Simba Ubingwa huu.

Hili linakuwa taji lake la nne (4) la Michuano hii ya Mapinduzi Cup wakati Wanalambalamba Azam FC wakiwa wamelichukua mara tano (5).

Mbali ya Ubingwa huo hii leo lakini pia beki wake Henock Inonga ameshinda zawadi ya mchezaji bora wa mechi hii ya fainali.

Aishi Manula ametwaa tuzo ya golikipa bora wa Michuano hiyo.

Mfungaji bora amekuwa Meddie Kagere wakati Mchezaji bora wa akichukua Sakho.

Related Articles

Back to top button